Wednesday, February 4, 2015


IMANI za kishirikina? Mshangao wa
aina yake umetokea nyumbani kwa Miss Tanzania 2006 asiyechuja, Wema
Abraham Sepetu ‘Madam’ baada ya kutupiwa hirizi getini kwake, Risasi
Mchanganyiko lina stori kamili.
Wananchi
wakishuhudia hirizi getini kwa Miss Tanzania 2006 asiyechuja, Wema
Abraham Sepetu ‘Madam’. Tukio hilo lililokusanya watu wapenda ‘ubuyu’
lilijiri alfajiri ya Jumamosi iliyopita,
nyumbani kwa mlimbwende huyo, Kijitonyama-Bwawani jijini Dar baada ya mapaparazi wetu kutonywa juu ya uwepo wa tukio hilo. 



TUJIUNGE NA CHANZO
“Njooni
hapa kwa Wema tumekuta mfuko mweusi wa nailoni, ndani yake una hirizi,
nazi zimeandikwa maandishi ya Kiarabu huku zikiwa zimevunjwavunjwa na
pia kuna picha ya Diamond ndani yake,” kilisema chanzo hicho.

MAPAPARAZI WATIA TIMU
Mapaparazi
wetu ambao walikuwa kwenye mizunguko yao kikazi, walitumia usafiri wa
pikipiki kwenda nyumbani hapo ambapo ndani ya dakika ‘sifuri’ walikuwa
wameshafika na kukuta vitu hivyo vikiwa vimezunguka na mashuhuda.


Wananchi wakizitazama kwa karibu zaidi hirizi hizo. KILA MTU ASEMA LAKE
Wakati
mapaparazi wetu walipokuwa wakidadisi juu nani aliyetupa kifurushi
hicho na sababu za kufanya hivyo, mashuhuda hao kila mmoja alieleza
lake.

“Sisi hatujui aliyetupa inaonekana atakuwa alikuja usiku
sana lakini inaonesha mtupaji atakuwa anataka Wema na Diamond warudiane
na ndiyo maana ameambatanisha na picha ya Diamond,” alisikika shuhuda
mmoja huku mwingine akidakia:
“Aliyetupa hapa atakuwa ameweka zindiko ili Diamond asirudiane tena na Wema. Atakuwa anataka Diamond aendelee na Zari.”

Katika hali ya kushangaza, mlinzi wa kampuni moja inayolinda nyumbani
kwa mlimbwende huyo, aliupiga teke na kuusambaratisha mfuko uliokuwa
umehifadhi vitu hivyo pamoja na hirizi.

MAPAPARAZI WAMGONGEA WEMA


Ili
kutaka kujua Wema amelichukuliaje tukio hilo, mapaparazi wetu waligonga
geti la Wema ambapo alitoka binti mmoja ambaye hakutaka kujitambulisha
jina lake na kuzungumza pasipo kufungua geti akiwa anachungulia kupitia
uwazi mdogo uliopo getini hapo.

Hizi
ndizo hirizi zilizokutwa getini kwa Wema zikiwa na picha ya 'Diamond'.
“He mimi sifungui, Madam (Wema) hayupo kwanza naogopa hivyo vitu si vya
kawaida, mimi nakwenda zangu ndani,” alisema binti huyo na kutoweka.

APIGIWA SIMU
Mapaparazi
wetu walimvutia waya Madam ambapo kilongalonga chake kiliita bila ya
kupokelewa, kesho yake (Jumamosi) mapaparazi walitia timu tena nyumbani
hapo na kuambiwa Madam hayupo huku simu yake ikiwa haipatikani.

WAHARIRI MZIGONI


Juzi,
Jumatatu wakati gazeti hili lilipokuwa linakwenda mitamboni, wahariri
wa gazeti hili walifunga safari hadi nyumbani kwa Wema na kugonga getini
kwake ambapo alitoka mtu wa karibu na Wema, Petit Man. Mazungumzo
yakawa hivi:
Petit: Yeah karibuni.

Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu. Wahariri: Tumekuja kumuona Madam, tumemkuta?
Petit: Mna miadi naye?
Wahariri: Hatuna ila we mwambie wahariri wa Global Publishers wanakuita.
Petit: Ok subirini.
(Baada ya sekunde 30) WEMA, PETIT WATOKA NA GARI
Wakati
wahariri wakiendelea kusubiri, Wema na Petit walitoka getini wakiwa na
gari aina ya Murano (lile la alilopewa Diamond) ndipo wakashusha kioo
ili waweze kuzungumza nao.
Mhariri: Mambo? Vipi mzima?
Wema: Mzima niambie.


Mhariri: Dakika mbili kidogo basi tuongee.
Wema: Nina haraka lakini.
Mhariri:
Hata dakika moja. Ni hivi, kuna picha tumeletewa na mapaparazi wetu
zinaonesha juzi hapa nyumbani kwako kuna mfuko ulitupwa hapa ukiwa na
hirizi na mazagazaga yanayosadikiwa kuwa ni ya kishirikina.

Mkali wa Bongo Fleva, 'Diamond Platnumz'. Wema: (Kwa mshtuko) Haaaah! Hapa...kwa...ngu.
Mhariri: Hapa kwako ndiyo tena ndani yake kuna picha ya Diamond.
Wema: Kwa kweli mimi...sijui...hata sielewi kama kuna kitu kama hicho kimetokea nyumbani kwangu.

MABAKI YAONEKANA
Wakati
wahariri wakiendelea na mazungumzo na Wema, waliona mabaki ya vipande
vya nazi pembeni ya geti hilo na kumuonesha Wema ambaye alizidi
kutaharuki.
“Haaah! Kweli jamani vipande vya nazi...sawa lakini mimi imani yangu haiamini hivi vitu,” alisema Wema.
Baada ya mazungumzo hayo, wahariri walimuaga Wema huku akiwa katika hali ya sintofahamu!
Na Global publishers

0 comments:

Post a Comment

Mr.Mputa

You are welcome in this blog you ca get us through..
Mobile+255717962720
+255767962720
Njombe Iringa Tanzania

TANGAZO

Karibuni katika Blog ya Jiliwaze hapa utapata mambo mbali mbali yakufunza na kuonya na kama unahitaji kutengenezewa email,facebook ac,page ama blog wasiliana nasi kupitia.. Phone:0717962720/0767962720 Email:mputae@yahoo.com :mputae@rocketmail.com

Popular Posts